• ePaper
Sunday, June 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MASHINA NI MOYO WA CCM – DK. ASHA-ROSE MIGIRO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 13, 2026
in Habari, Kitaifa
0
MASHINA NI MOYO WA CCM – DK. ASHA-ROSE MIGIRO

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Asha-Rose Migiro

0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Asha-Rose Migiro, amesema uimara wa CCM unatokana na wanachama wake kujitokeza kikamilifu katika mikutano ya chama kwa kuwashirikisha wanachama wa CCM pamoja na wananchi wasiokuwa wanachama, hali inayokifanya chama hicho kuendelea kuwa imara na chenye mvuto kwa Watanzania.

Akizungumza na mabalozi wa mashina na wanachama wa CCM katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam, Dk. Migiro amesema ubora wa CCM unatokana na siasa zake za kujenga hoja na kuimarisha imani ya kudumu kwa wananchi, akisisitiza kuwa misingi hiyo imeifanya CCM kuwa chama chenye uthabiti wa kisiasa kwa miaka mingi.

Ameeleza kuwa chama kimeweka utaratibu madhubuti wa kuimarisha vikao vya mashina kwa kukutana mara kwa mara, akibainisha kuwa mikutano hiyo ni nyenzo muhimu ya kusikiliza wananchi, kujenga mshikamano na kuimarisha demokrasia ya ndani ya chama.

Dk. Migiro amesisitiza kuwa itikadi ya CCM itaendelea kujengwa juu ya misingi ya utu, ujamaa na kujitegemea kama inavyobainishwa kwenye kauli mbiu ya chama “Kazi na Utu, Tunasonga Mbele”, akieleza kuwa dhamira ya CCM ya kushika Dola inalenga kujenga utu wa Mtanzania kwa kuboresha maisha yao kupitia ujenzi wa miundombinu, hospitali na huduma nyingine za kijamii.

Akifafanua nafasi ya mashina ndani ya chama, alisema licha ya kuonekana kama ngazi ndogo ya uongozi, mashina ndiyo nguzo kuu inayobeba uimara na umadhubuti wa CCM. “Mashina ni moyo wa Chama Cha Mapinduzi,” amesisitiza.

Aidha, ametoa wito kwa wanachama kushiriki kikamilifu katika vikao vya mashina na kuendelea kutangaza maendeleo yanayopatikana chini ya uongozi wa CCM, huku akiwataka mabalozi kuenzi alama za chama, kuendesha mikutano kwa nidhamu na kuwashirikisha wananchi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Previous Post

RAIS DK. SAMIA AHIMIZA AMANI, MSHIKAMANO

Next Post

JASHO LIMEMWAGIKA

Next Post
JASHO LIMEMWAGIKA

JASHO LIMEMWAGIKA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WASOMI, WACHAMBUZI WATOA NENO SERIKALI KUWEZESHA VIJANA

WASOMI, WACHAMBUZI WATOA NENO SERIKALI KUWEZESHA VIJANA

6 months ago
USAFIRISHAJI MAJINI KUFUNGUA UCHUMI WA MWANZA NA TAIFA

USAFIRISHAJI MAJINI KUFUNGUA UCHUMI WA MWANZA NA TAIFA

2 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

    RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • AFRIKA KUCHOCHEA UTUNZAJI MAZINGIRA KUPITIA NISHATI SAFI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWAKINYO AOMBA RADHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, SIMBA NI KIVINGINE ZAIDI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MEXICO YAANZA KWA KISHINDO WC, KADI ZATEMBEA HATARI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?