• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

KAPOMBE, DUCHU WATOA MSIMAMO SIMBA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 23, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
KAPOMBE, DUCHU WATOA MSIMAMO SIMBA
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

IKIWA imesalia siku moja ili kushuka dimbani katika mchezo wake dhidi ya Esperance De Tunis ya Tunisia, wachezaji wa Simba wametoa msimamo kuwa watahakikisha wanashinda ili kuwapa furaha mashabiki wao.

Simba ipo nchini Tunisia kwa ajili ya mchezo wake wa tatu wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa katika Uwanja wa Stade Olympique Hammadi mechi zote zikichezwa saa 1:00 usiku.

Wekundu hao wa msimbazi, wapo kundi D ikiwa inaburuza mkia huku  Esperance ikiwa na pointi mbili  baada ya kupata sare katika mechi mbili za awali na kushika nafasi ya tatu.

Wakizungumza jana  kutoka nchini Tunisia kwa nyakati tofauti, nyota wa timu hiyo, Shomari Kapombe alisema wanajua wanatakiwa kushinda ili kuwapa furaha mashabiki wao baada ya hivi karibuni kupata matokeo ambayo si mazuri.

“Hatujapata ushindi katika mechi zetu mbili, lakini tutahakikisha tunapambana ili kushinda katika mchezo huu dhidi ya  Esperance na kupata mwanga wa kusonga mbele,”alisema.

Mlinzi huyo alifafanua kuwa wanajua mchezo huo utakuwa mgumu wenye ushindani mkubwa lakini hawatakubali kupoteza.

“Tutajitoa kwa hali na mali ili kupata ushindi, lengo tusonge mbele huku tukiwapa furaha mashabiki wetu,” alisema

Kapombe aliongeza kwamba  watatumia uzoefu waliokuwa nao katika mashindano ya kimataifa ili kupata ushindi na kujizolea pointi tatu muhimu.

“Utakuwa mchezo mgumu na wenye changamoto kubwa lakini tutapambana kufa au kupona ili kupata ushindi, lengo letu ni kupata pointi tatu,” alisema Kapombe.

David Kameta ‘Duchu’ alisema kuwa wachezaji wote wamejipanga kupambana kwa jasho na damu ili kupata ushindi.

Alisema kwamba wanawaheshimu wapinzani wao na wataingia katika mchezo huo, wakicheza kwa nidhamu kubwa ili kushinda.

“Tunaenda katika mchezo mgumu na wenye changamoto kubwa, hatutakubali kupoteza tutapambana kwa jasho na damu ili kupata matokeo mazuri,” alisema Duchu.

Hata hivyo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally alisema kuwa timu yao imefika salama Tunisia na tayari wameanza maandalizi kwa ajili ya mchezo huo muhimu.

“Timu imefika salama Tunisia na mwalimu ameshaanza programu ya mazoezi kwa ajili ya mchezo huo muhimu, wachezaji wote wana morari ya kutosha kuhakikisha wanapata ushindi na kurejea na pointi tatu nyumbani,” alisema Ahmed.

Baada ya mchezo huo, Simba itarejea nyumbani kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Esperance utakaochezwa Februari Mosi, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Previous Post

AL AHLY, YANGA UBORA UTAONGEA

Next Post

BONDIA DULLAH MBABE AWAITA MASHABIKI

Next Post
BONDIA DULLAH MBABE AWAITA MASHABIKI

BONDIA DULLAH MBABE AWAITA MASHABIKI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

PBPA YAAGIZWA KUHARAKISHA UPOKEAJI NA USAZAMBAZAJI WA MAFUTA NCHINI

PBPA YAAGIZWA KUHARAKISHA UPOKEAJI NA USAZAMBAZAJI WA MAFUTA NCHINI

3 weeks ago
WATOTO HAWASTAHILI KUCHOMWA VIGANJA KWA KUDOKOA NYAMA

WATOTO HAWASTAHILI KUCHOMWA VIGANJA KWA KUDOKOA NYAMA

3 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?