• ePaper
Thursday, July 30, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DK. MWIGULU ATAKA USHIRIKIANO WA KIKANDA MAPAMBANO DHIDI YA SARATANI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 12, 2026
in Habari, Kitaifa
0
DK. MWIGULU ATAKA USHIRIKIANO WA KIKANDA MAPAMBANO DHIDI YA SARATANI
0
SHARES
13
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI MKUU, Dk. Mwigulu Nchemba amesema kuwa Afrika haiwezi kushinda vita dhidi ya saratani ikiwa kila nchi itafanya kazi peke yake.

Amesema kuwa ili kufikia malengo ya mapambano dhidi ya saratani, kunahitajika kuwepo kwa ushirikiano wa kikanda na wa bara zima katika utafiti, mafunzo, kubadilishana wataalamu na kubadilishana rasilimali, teknolojia pamoja na uzoefu.

Ametoa wito huo leo Alhamisi (Februari 12, 2026) alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya miaka 30 ya Taasisi ya Saratani Ocean Road, yanayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Tanzania iko tayari kushirikiana na nchi zote za Afrika na kupitia Taasisi ya Saratani Ocean Road tutaendelea kuwa kituo cha ushirikiano wa kikanda na bara zima katika mapambano dhidi ya saratani”.

Dk. Mwigulu amesema kuwa kupitia simulizi za machapisho ya kitafiti na sayansi ambazo wataalamu wa Taasisi ya Saratani Ocean Road na Tanzania kwa ujumla wameyafanya, yamekuwa na mchango mkubwa ndani na nje ya nchi kisera na kiutendaji katika mapambano dhidi ya saratani.”

Katika hatua nyingine, Dk. Mwigulu ameiagiza Wizara ya Afya kuandaa mkakati madhubuti wa kupunguza idadi ya wagonjwa wapya wa saratani ili kupunguza athari kwa rasilimaliwatu, uchumi na ustawi wa Taifa kwa ujumla.

“Kutokana na tahadhari ya wataalamu wa afya kutoka Shirika la Afya Duniani kuhusu ugonjwa wa saratani kuongezeka kwa zaidi ya asilimia 60 ifikapo mwaka 2030, Wizara ya Afya mnapaswa kuandaa mikakati ya kupunguza idadi ya wagonjwa wapya.”

Previous Post

WADAU WAMPA TANO RAIS DK. SAMIA KUIHESHIMISHA TAIFA STARS

Next Post

RAIS DK. SAMIA KUNG’ARA AU

Next Post
RAIS DK. SAMIA KUNG’ARA AU

RAIS DK. SAMIA KUNG’ARA AU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

USAFIRISHAJI MAJINI KUFUNGUA UCHUMI WA MWANZA NA TAIFA

USAFIRISHAJI MAJINI KUFUNGUA UCHUMI WA MWANZA NA TAIFA

4 months ago
KIBANO KIKALI WALIOZIMA ‘X-RAY’ TEMEKE

KIBANO KIKALI WALIOZIMA ‘X-RAY’ TEMEKE

7 months ago

Popular News

  • MVUTANO MAZISHI YA WAMBURA WAFIKA KORTINI, DALILI ZA MARIDHIANO ZACHOMOZA

    MVUTANO MAZISHI YA WAMBURA WAFIKA KORTINI, DALILI ZA MARIDHIANO ZACHOMOZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA ATAJA SIFA ZA MAWASILIANO SERIKALINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • 50 BORA ‘FORM SIX’ KUSOMA AI NJE YA NCHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DHAHABU YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI 1.2/- YAKAMATWA IKITOROSHWA DAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA ATAKA UADILIFU, USHIRIKIANO NA MATOKEO KWA VIONGOZI WAPYA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?