• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

YANGA YAOMBA KUOMBEWA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 13, 2026
in Burudani, Habari, Michezo
0
YANGA YAOMBA KUOMBEWA
0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

UONGOZI wa Klabu ya Yanga umeziomba timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Championship, kuiombea timu yao, ifuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).

Yanga inatarajiwa kushuka dimbani keshokutwa katika mchezo wa mwisho hatua ya makundi ya CAFCL dhidi ya JS Kabylie ya Algeria utakaochezwa katika Uwanja wa New Amaan Complex, visiwani Zanzibar kuanzia saa 1:00 usiku.

Timu hiyo yenye Makao Makuu yake mitaa ya Twiga na Jangwani, inahitaji ushindi wa tofauti ya mabao mawili mbele ya Kabylie, iliyopoteza tumaini la kusonga mbele kupitia kundi B linaloongozwa na Al Ahly ya Misri ikiwa na pointi tisa.

Katika msimamo nafasi ya pili inashikiliwa na AS FAR yenye pointi nane, Yanga nafasi ya tatu kwa pointi tano huku Kabylie ikiburuza mkia ikiwa na pointi tatu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda Zanzibar, Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, alisema kwa hali iliyopo hivi sasa hakuna timu nyingine nchini ambayo angalau ina  uhakika wa kusonga mbele hatua ya makundi isipokuwa Yanga pekee.

“Tunaomba timu zote watuombee ili Yanga iheshimishe Tanzania, angalu kama nchi tuwe na timu moja katika hatua ya robo fainali katika michuano ya kimataifa,” alisema Kamwe.

Ofisa huyo alisema kuwa timu yao haitakuwa na mapumziko na badala yake inaendelea na maandalizi kwa ajili ya mechi yao ya mwisho dhidi ya JS Kabylie.

Alifafanua kuwa hawana hofu na timu yao kwani wanakwenda kucheza uwanja ambao wameuzoea, hivyo watapambana mwanzo hadi mwisho kusaka ushindi.

Kamwe alisema kuwa wachezaji wote wana morari ya kutosha kuelekea katika mchezo huo muhimu kwani lengo kubwa ni kupata ushindi wa mabao mengi na hilo linawezekana.

“Niwaambie tu mashabiki na wapenzi wa timu yetu wanatakiwa kujaa kwa wingi uwanjani ili kuweza kuisapoti timu yao na kuwaongezea morari wachezaji wanapokuwa uwanjani,” alisema Kamwe.

Previous Post

SIMBASC KUWEKA HESHIMA CAFCL

Next Post

SIKU 100 ZA RAIS DK. MWINYI IKULU ZANZIBAR

Next Post
SIKU 100 ZA RAIS DK. MWINYI IKULU ZANZIBAR

SIKU 100 ZA RAIS DK. MWINYI IKULU ZANZIBAR

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

YANGA, SINGIDA, MLANDEGE MZIGONI TENA KIMATAIFA

YANGA, SINGIDA, MLANDEGE MZIGONI TENA KIMATAIFA

7 months ago
MRADI WA BILIONI 18.9/- BUKOBA WAMPA SIFA RAIS DK. SAMIA

MRADI WA BILIONI 18.9/- BUKOBA WAMPA SIFA RAIS DK. SAMIA

3 weeks ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?