• ePaper
Friday, April 17, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

YANGA YATUMA SALAMU MSIMBAZI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 26, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
YANGA YATUMA SALAMU MSIMBAZI
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

YANGA imetuma salamu kwa watani wao jadi Simba, baada ya kuinyanyasa  JKT Tanzania  kwa kuifunga 5-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam.

Ushindi huo ni salamu tosha kwa Wekundu wa Msimbani kueleka katika mchezo wa ‘dabi’ utakaochezwa Machi Mosi, mwaka huu katika Uwanja wa New Amaani Complex, Zanzibar.

Baada ya matokeo hayo, Yanga inaongoza ligi hiyo ikiwa na alama 28, ikiishusha JKT Tanzania hadi nafasi ya pili katika msimamo kwa tofauti ya mabao  ya kufunga na kufungwa.

Yanga imecheza mechi 10  na JKT  Tanzania imeshuka dimbani mara 17 na ina poin ti 28 katika ligi hiyo yenye ushindani mkubwa.

Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zote zikipambana kusaka ushindi lakini dakika ya sita, Mohamed Hussein ‘Tshabalala alifunga bao la kuongoza  kwa shuti, baada ya kumalizia pasi safi kutoka kwa Dube Abuya.

Mpira uliendelea kwa kasi na dakika ya 20 kipa wa JKT , Ramadhan Chalamanda alifanya kazi ya ziada kupangua shuti la Israel Mwenda, baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Mudathir Yahya.

JKT Tanzania walikosa bao, dakika ya 41 ya mchezo huo kupitia kwa mchezaji wake, Paul Peter ambaye alifumua shuti lililotoka nje ya lango la Yanga.

Dakika ya 60, Yanga ilipata bao la pili kupitia kwa Laurindo Aurelio ‘Dupe’ baada ya kupiga mpira kwa kichwa kufuatia kupokea pasi kutoka kwa Israel Mwenda.

Kabla hawajamaliza kushangilia dakika ya 62, Mudathir Yahya alipachika bao la tatu baada ya kupiga shuti kali lililokwenda wavuni moja kwa moja, Mudathir alimalizia mpira uliogongwa mwamba ambao ulipigwa na Prince Dube.

Prince Dube katika dakika ya 85 alifunga bao la nne kwa shuti  na dakika ya 89, Yanga ilipata bao la tano kupitia kwa Shekhani Khamis.

Yanga iliwakilishwa na Djigui Diarra, Ibrahim Abdulla, Dikson Job, Maxi Nzengeli, Mudathir Yahya, Israel Mwenda, Allan Okello, Mohamed Hussein, Laurindo Dilson/Mwanengo, Prince Dube na  Duke Abuya/.

JKT Tanzania: Ramadhani Chalamanda, Anuary Kilemile, Karimu Mfaume, Hassan Nassor, Sospeter Bajana, Salehe Karabaka, Edson Katanga, Ally Msengi, Pascal Mussa, Paul Peter na Mohemed Bakari.

Previous Post

WATU 120, 780 KUMCHAGUA MBUNGE JIMBO LA PERAMIHO

Next Post

SEKTA YA UCHUKUZI YAPAA

Next Post
SEKTA YA UCHUKUZI YAPAA

SEKTA YA UCHUKUZI YAPAA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SERIKALI YAONDOA HOFU UKOSEFU ARV’S

SERIKALI YAONDOA HOFU UKOSEFU ARV’S

5 months ago
TPLB YAGUSIA WAZO LA FIFA USAWA WA KALENDA

TPLB YAGUSIA WAZO LA FIFA USAWA WA KALENDA

4 months ago

Popular News

  • KIGOGO CHAUMMA ‘AIPA TANO’ TUME YA JAJI CHANDE

    KIGOGO CHAUMMA ‘AIPA TANO’ TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MUYUNGI ASISITIZA WANANCHI KUFANYA BIASHARA YA KABONI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KAMATI YA UTALII, BIASHARA NA KILIMO BARAZA LA WAWAKILISHI YADHAMIRIA MAMLAKA YA VIPIMO ZANZIBAR IFIKIE VIWANGO VYA WMA BARA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • LAZARUS CHAKWERA AMALIZA ZIARA YA SIKIU 9 NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA KISHINDO SGR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?