• ePaper
Sunday, June 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

SINGIDA, SIMBA BALAA ZITO LEO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 11, 2026
in Burudani, Habari, Michezo
0
SINGIDA, SIMBA BALAA ZITO LEO
0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAKATI Simba ikihitaji kupunguza idadi ya pointi ilizoachwa na kinara Yanga, kikosi cha Singida Black Stars kitaingia katika mtanange wa leo, kuvunja mwiko wa kutoshinda mechi mbili mfululizo dhidi ya Wekundu hao wa Msimbazi katika Ligi Kuu Bara.

Singida Black Stars itachuana na Simba leo saa 10:00 jioni katika Uwanja wa Airtel uliopo  mjini  Singida.

Katika pambano hilo, Simba itahitaji alama tatu kusogea zaidi katika mbio za kuwania ubingwa dhidi ya kinara Yanga wakati Singida ikiwa na kibarua cha kuvunja mwiko wa kutoifunga Simba katika mechi mbili msimu uliopita.

Katika mitanange hiyo miwili msimu uliopita, Simba ilianza kwa ushindi wa bao 1-0 ugenini kabla ya kushinda 1-0 nyumbani katika ligi hiyo.

Kwa mujibu wa msimamo wa ligi hiyo, Simba ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 24 baada ya kushuka dimbani mara 11, imeshinda mechi saba,  imetoka sare mara tatu na kufungwa moja, ikiachwa alama nane na kinara Yanga iliyocheza mechi 12.

Wekundu hao wa Msimbazi wamefunga mabao 18 na kuruhusu mabao manne.

Kwa upande wa Singida Black Stars ipo nafasi ya tisa ikiwa na alama 19 baada ya kucheza mechi 12, ikishinda tano, sare nne na kufungwa tatu, ikipachika mabao 11 na kuruhusu mabao 11.

Kocha wa Singida Black Stars, David Ouma alisema kikosi chao kipo fiti na kinahitaji alama tatu katika mechi hiyo.

“Matarajio yetu ni kutumia vyema uwanja wetu wa nyumbani, tunajua ubora wa mpinzani wetu, lakini lengo letu ni kupata ushindi, tutahakikisha tunacheza kwa ubora zaidi,”

Kocha wa Simba, Steve Barker, alikiri ubora wa Singida Black Stars, lakini ana imani kikosi chake kitavuna pointi tatu.

“Ni mechi nzuri sana, tumetoka kupata sare mbili, sasa tunahitaji kushinda ili kurejea katika ubora, Singida ni timu nzuri, lakini niwaahidi tu mashabiki kwamba tutafanya kila linalowezekama kupata ushindi,” alisema.

Mchezo mwingine utakaopigwa leo utakuwa kati ya Azam FC na Dodoma Jiji utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma saa 1:15 usiku.

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Kassim Liogope, alikiri mechi hiyo itakuwa ngumu lakini anaamini timu yake itapata ushindi.

“Tunajua tunakwenda kukutana na mshindani wa aina gani, bahati nzuri tumepata kuwaona Dodoma Jiji wakicheza, ni timu imebadilika, ninaamini tutakuwa na mechi nzuri,” alisema.

Kocha wa Dodoma Jiji, Aman Josiah alisema amekiandaa vyema kikosi chake kuwania pointi  tatu na japokuwa kumkosa mchezaji Abdi Banda anayetumikia adhabu ya kukosa mechi tatu, itakiathiri kikosi hicho.

Previous Post

MIGOGORO ARDHI MFUPA MGUMU

Next Post

RAIS DK. SAMIA AMUASILI MTOTO MCHANGA ALIYETELEKEZWA NZEGA

Next Post
RAIS DK. SAMIA AMUASILI MTOTO MCHANGA ALIYETELEKEZWA NZEGA

RAIS DK. SAMIA AMUASILI MTOTO MCHANGA ALIYETELEKEZWA NZEGA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SIMULIZI YA KUSIKITISHA ANAYEDAIWA KUUA MKE

SIMULIZI YA KUSIKITISHA ANAYEDAIWA KUUA MKE

4 months ago
PANTEV ATAJA SABABU KUPOTEZA CAFCL

PANTEV ATAJA SABABU KUPOTEZA CAFCL

6 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

    RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • AFRIKA KUCHOCHEA UTUNZAJI MAZINGIRA KUPITIA NISHATI SAFI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWAKINYO AOMBA RADHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, SIMBA NI KIVINGINE ZAIDI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MEXICO YAANZA KWA KISHINDO WC, KADI ZATEMBEA HATARI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?