• ePaper
Sunday, September 13, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

ZIARA YA KIHONGOSI MWANZA YAREJESHA MATUMAINI KWA WANANCHI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 13, 2026
in Habari, Kitaifa, Siasa
0
ZIARA YA KIHONGOSI MWANZA YAREJESHA MATUMAINI KWA WANANCHI
0
SHARES
12
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

ZIARA ya Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenan Kihongosi, mkoani Mwanza, imerejesha matumani kwa wananchi wa jiji hilo.

Kihongosi ambaye amefanya mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Furahisha, Nyamagana mkoani humo, ametatua baadhi ya changamoto za wananchi papo kwa papo.

Miongoni mwa wananchi waliotatuliwa changamoto zao ni mama mmoja aitwaye Happiness Benedict, aliyeomba msaada wa matibabu kutokana na tatizo la kusagika kwa nyonga lililomsumbua kwa takribani miaka mitano.

Amesema madaktari walimwambia anatakiwa kufanyiwa upasuaji, ambapo gharama ya matibabu inakadiriwa kufikia zaidi ya Sh. milioni 14.

Happiness amesema awali alikuwa na bima ya afya lakini ilikwisha muda wake, hivyo sasa hana uwezo wa kumudu gharama za matibabu.

“Hatuwezi kushindwa kupata Sh. milioni 14 au 15 kwa ajili ya kuokoa maisha ya mtu, tutashughulikia suala hili,” amesema Kihongosi.

Baada ya kumalizika mkutano, Kihongosi alimwita DMO kumhabarisha kuwa amepokea kiasi cha Sh. milioni 15 kupitia akaunti ya NMB kwa ajili ya matibabu ya Happiness.

Pia, amesaidia kupatikana kwa ada ya mwanafunzi wa chuo ambaye aliomba msaada katika mkutano huo ili aweze kuendelea na masomo, na fedha hizo zilipatikana hapo hapo.

Previous Post

IBENGE FURAHA TELE

Next Post

WATANZANIA SABA WAWASILI NCHINI KUTOKEA IRAN

Next Post
WATANZANIA SABA WAWASILI NCHINI KUTOKEA IRAN

WATANZANIA SABA WAWASILI NCHINI KUTOKEA IRAN

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. MWINYI AJAWA MATUMAINI KIBAO

DK. MWINYI AJAWA MATUMAINI KIBAO

11 months ago
MAKONDA ASISITIZA KUTOVUMILIA WAKANDARASI WAZEMBE AFCON

MAKONDA ASISITIZA KUTOVUMILIA WAKANDARASI WAZEMBE AFCON

7 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA NI KIONGOZI WA MATOKEO

    RAIS DK. SAMIA NI KIONGOZI WA MATOKEO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA, NDEJEMBI TURUFU YA MAENDELEO KWA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI AONYA, ATOA SIKU 60 WENYE SILAHA HARAMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NDEJEMBI MZIGONI RASMI, AKEMEA KAZI KWA MAZOEA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUME MIPANGO, NIRC WAJADILI UBORA MIRADI YA UMWAGILIAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?