• ePaper
Sunday, June 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WATANZANIA SABA WAWASILI NCHINI KUTOKEA IRAN

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 13, 2026
in Habari, Kitaifa
0
WATANZANIA SABA WAWASILI NCHINI KUTOKEA IRAN
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WATANZANIA  Saba waliokuwa nchini Iran wamewasili nchini leo Machi 13, 2026, kufuatia operesheni ya uokozi iliyoratibiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Watanzania hao wamewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 8:40 usiku kwa kutumia Shirika la Ndege la Uturuki, wakitokea nchini Uturuki ambako walipokelewa awali baada ya kuvuka mpaka wa nchi kavu wakitokea nchini Iran.

Watanzania hao wamepokelewa na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Abdallah Kilima, pamoja  na maafisa wengine wa wizara.

Mapokezi ya Watanzania hao yaligubikwa na hisia za faraja kutoka kwa ndugu na jamaa waliokuwa wakihofia usalama wa wapendwa wao.

Wakizungumza baada ya kuwasili uwanjani hapo, Watanzania hao wameishukuru serikali kwa kuratibu zoezi la kurejeshwa kwao nchini.

Serikali ya Tanzania ilichukua hatua za dharura kulinda maisha ya raia wake waliokuwa nchini humo kwa masomo na shughuli nyingine.

Safari ya kurejea nyumbani kwa Watanzania hao ilianzia kwenye mpaka wa Razi (Iran) na kufika Kapıkule (Uturuki) mnamo Machi 11, 2026 na kupokelewa na Balozi wa Tanzania  nchini Uturuki, Iddi Seif Bakari na Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania.

Previous Post

ZIARA YA KIHONGOSI MWANZA YAREJESHA MATUMAINI KWA WANANCHI

Next Post

RAIS DK. SAMIA AWALILIA WATUMISHI WALIOFARIKI AJALI YA BOTI KIGOMA

Next Post
RAIS DK. SAMIA AWALILIA WATUMISHI WALIOFARIKI AJALI YA BOTI KIGOMA

RAIS DK. SAMIA AWALILIA WATUMISHI WALIOFARIKI AJALI YA BOTI KIGOMA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MIGIRO KATIBU MKUU WA  KWANZA MWANAMKE NA MIKAKATI YA KUIMARISHA MASHINA KATIKA MITAA

MIGIRO KATIBU MKUU WA  KWANZA MWANAMKE NA MIKAKATI YA KUIMARISHA MASHINA KATIKA MITAA

5 months ago
WADAU MICHEZO WAMTUMIA SALAMU WAZIRI MAKONDA

WADAU MICHEZO WAMTUMIA SALAMU WAZIRI MAKONDA

5 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

    RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • AFRIKA KUCHOCHEA UTUNZAJI MAZINGIRA KUPITIA NISHATI SAFI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWAKINYO AOMBA RADHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, SIMBA NI KIVINGINE ZAIDI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MEXICO YAANZA KWA KISHINDO WC, KADI ZATEMBEA HATARI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?