• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

DIARRA MTEGONI TUZO KIPA BORA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 31, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
DIARRA MTEGONI TUZO KIPA BORA
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

ABDUL DUNIA Na ZIANA BAKARI

IKIWA ni siku nne tangu kipa wa Yanga, Djigui Diarra kufungiwa mechi tatu, adhabu hiyo inaweza kubadili taswira katika vita ya kuwania tuzo ya kipa bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Diarra alifungiwa mechi hizo na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) Ijumaa iliyopita, kufuatia mlinda lango huyo raia wa Mali kufanya kosa la kumshambulia mwamuzi wa kati wa mechi dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya mtanange huo kumalizika katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Kutokana na adhabu hiyo, Diarra anatarajiwa kukosa mechi dhidi ya Tanzania Prisons, Pamba Jiji na Mbeya City.

Hatua ya kipa huyo kukosa mechi tatu zijazo za Yanga, inaweza kuwarudisha mchezoni makipa mbalimbali na kuongeza ushindani katika vita ya kipa bora wa Ligi Kuu msimu huu.

Kwa mujibu wa kanuni, tuzo ya kipa bora inakwenda kwa mlinda lango ambaye hajaruhusu bao katika mechi nyingi zaidi.

Katika ligi hiyo, Diarra ndiye kinara akiwa amecheza mechi 10 bila ya kuruhusu bao huku akifuatiwa na Aishi Manula wa Azam FC (6), Erick Johora wa Mashujaa (6), Jean Noel wa TRA United (6).

Wengine ni Djibrilla Kassali wa Simba (5), Zuberi Foba wa Azam FC (5), Yona Amosi kutoka Pamba Jiji (5), Ally Salim wa Dodoma Jiji (5) na Mussa Mbisa wa Tanzania Prisons (5).

Kama makipa hao watacheza vizuri katika mechi tatu zijazo na kutoruhusu bao ni wazi ushindani mpya utazaliwa katika mbio za kuwania tuzo ya kipa bora wa michuano hiyo msimu huu.

Kocha wa Buguruni Youth, Omary Mbweze alisema mechi tatu ni nyingi kwa kipa hivyo adhabu hiyo inaweza kumgharimu kwa kuwa wenzake wanaweza kufanya vyema zaidi na yeye akakosa ufiti wa mechi atakaporejea dimbani.

“Kukosa mechi tatu ni pigo, inaweza kusababisha kukosa utimamu katika mechi hivyo ubora wake, unaweza kupungua,” Mbweze.

Kocha wa Mbeya City, Mecky Maxime, alisema haoni sababu ya kipa huyo kumuathiri kwa kuwa atapata muda mwingi zaidi wa kujipanga ili kuwa bora zaidi.

“Kukosa mechi tatu ni jambo la kawaida na nafikiri atapata muda wa kupumzika zaidi, lakini ni suala la kawaida katika mpira,”  alisema Mexime.

Mbali na kufungiwa mechi tatu, pia Diarra ametakiwa kulipa sh. milioni nne kwa makosa mawili tofauti ambapo kila kosa linagharimu faini ya sh. milioni mbili.

Previous Post

CHANETA IMANI KIBAO NA TUME HURU YA UCHUNGUZI

Next Post

DK. MWIGULU MGENI RASMI MTOKO WA CHRISTINA SHUSHO

Next Post
DK. MWIGULU MGENI RASMI MTOKO WA CHRISTINA SHUSHO

DK. MWIGULU MGENI RASMI MTOKO WA CHRISTINA SHUSHO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

CARDINAL PENGO AFARIKI DUNIA

CARDINAL PENGO AFARIKI DUNIA

2 months ago
WASIRA : VIJANA MSIKUBALI KUTUMIKA KUVURUGA AMANI

WASIRA : VIJANA MSIKUBALI KUTUMIKA KUVURUGA AMANI

4 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?