• ePaper
Wednesday, April 22, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

NYAMBUI AFUNGUKAAMANI KATIKA MICHEZO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 16, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
NYAMBUI AFUNGUKAAMANI KATIKA MICHEZO
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

‎Na VICTOR MKUMBO
‎
‎MWANARIADHA mkongwe na kocha wa mchezo huo, Suleiman Nyambui, amesema michezo na utamaduni kwa ujumla ina nafasi kubwa ya kutunza na kuendeleza amani iliyopo nchini.
‎
‎Akizungumza jijini Dar es Salaam, Nyambui alisema michezo na utamaduni ina sehemu kubwa ya kudumisha amani kwani inakutanisha watu wengi na wa matabaka tofauti kwa wakati mmoja.

“Hata katika kamati ya michuano ya Olimpiki, huwa hawachagui matabaka na badala yake mashindano hayo hushirikisha nchi zote bila kujali itikati,” alisema.
‎
‎Alifafanua kuwa kwa Tanzania michezo yote ikiwemo ngoma za asili zina nafasi ya kipekee katika kuimarisha amani kwa kuwafanya watu kufurahi kwa pamoja.
‎
‎”Michezo ina nafasi kubwa katika kudumisha amani na umoja uliyopo nchini.
‎
‎” Pia burudani husaidia kuwaweka wadau sehemu moja na kufurahia ngoma zikiwemo za asili, kitu ambacho kimekuwa utamaduni wa Watanzania kwa miaka mingi,” alisema Nyambui.
‎
‎Nyambui alisisitiza kwamba, serikali bado ina nafasi ya kuanzisha mashindano ya michezo na burudani kuanzia ngazi za awali ,kuhakikisha watu wote wanapata muda wa kuburudika.
‎
‎Alisema kurejeshwa kwa mashindano hayo, kutawafanya vijana kujikita katika utamaduni zaidi na kuachana na mambo ya makundi yasiyofaa kwa jamii.
‎
‎”Tusisubiri hadi viongozi waseme wana shughuli fulani ndipo tuanze kutafuta wacheza ngoma, wanatakiwa kuandaliwa kwa mashindano kuanzia ngazi za awali kuhakikisha wanapatikana washindi wa kitaifa.
‎
‎”Hii pia itasaidia kupunguza au kumaliza vijana ambao wanaingia katika makundi yasiyofaa kwa jamii,” alisema Nyambui.

Previous Post

YANGA, MBEYA CITY KAZI IPO LEO

Next Post

MAFANIKIO YA KISHINDO SGR

Next Post
MAFANIKIO YA KISHINDO SGR

MAFANIKIO YA KISHINDO SGR

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TANZANIA, UGANDA KATIKA TAKWIMU

TANZANIA, UGANDA KATIKA TAKWIMU

4 months ago
AHUKUMIWA KUNYONGWA KWA KUTIWA HATIANI KUUA

AHUKUMIWA KUNYONGWA KWA KUTIWA HATIANI KUUA

5 months ago

Popular News

  • DK.NCHIMBI AMTAJA ASKOFU MFUMBUSA NGUZO YA UMOJA

    DK.NCHIMBI AMTAJA ASKOFU MFUMBUSA NGUZO YA UMOJA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SITAWAANGUSHA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA YATIMUA VUMBI CAF, SIMBA MMH

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AMPA TANO SIMBU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAAJABU YA DP WORLD SIKU 730 BANDARINI DAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?