• ePaper
Wednesday, April 22, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

YANGA, MBEYA CITY KAZI IPO LEO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 16, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
YANGA, MBEYA CITY KAZI IPO LEO
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

KOCHA wa Yanga, Pedro Goncalves, amesema wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo dhidi ya Mbeya City leo, kujiweka nafasi nzuri kutimiza malengo waliyojiwekea.

Yanga itashuka dimbani kumenyana na Mbeya City saa 12:30 jioni katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa Uwanja wa KMC, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam, Pedro alisema wanaiheshimu Mbeya City kutokana na ubora wake lakini hawatakubali kupoteza mechi hiyo.

Pedro alisema amepata muda wa kufanya maandalizi na kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo uliopita kufanya vizuri katika mchezo huo muhimu.

“Tumejipanga vizuri kuhakikisha tunapata ushindi, kila mchezo kwetu ni fainali, tunahitaji kupata pointi tatu muhimu kusalia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu,” alisema.

Kocha huyo alisema wachezaji wake wapo vizuri isipokuwa wataendelea kumkosa straika Prince Dube na Laurindo Aurelio ‘Depu’ ambao bado ni majeruhi.

Kocha wa Mbeya City, Mecky Mexime, alisema anajua mchezo utakuwa mgumu lakini wataingia katika mtanange huo bila ya kuihofia Yanga.

Alisema ni mchezo mgumu watacheza kwa akili na kuwaheshimu wapinzani wao lakini wao pia wanamitego yao kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

Mexime aliwataka mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kujaa kwa wingi uwanjani kuwapa sapoti na kuangalia timu yao jinsi ilivyobadilika kwa sasa.

Mchezaji wa Mbeya City Sudi Dondola, alisema kila mchezaji amejipanga vizuri kuhakikisha wanapambana na Yanga kupata ushindi.

Katika msimamo wa Ligi Kuu, Yanga ipo kileleni ikiwa na pointi 44 huku Mbeya City ikishika nafasi ya 12 kwa pointi 17, kila moja ikishuka dimbani mara 18.

Previous Post

RAIS DK. MWINYI AFICHUA KUWA NA KIPAJI CHA SOKA

Next Post

NYAMBUI AFUNGUKAAMANI KATIKA MICHEZO

Next Post
NYAMBUI AFUNGUKAAMANI KATIKA MICHEZO

NYAMBUI AFUNGUKAAMANI KATIKA MICHEZO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MGODI WA KIHISTORIA WA NIOBIUM KUJENGWA MKOANI MBEYA

MGODI WA KIHISTORIA WA NIOBIUM KUJENGWA MKOANI MBEYA

4 weeks ago
OUNAHI TEGEMEO MOROCCO AFCON 2025

OUNAHI TEGEMEO MOROCCO AFCON 2025

4 months ago

Popular News

  • YANGA YATIMUA VUMBI CAF, SIMBA MMH

    YANGA YATIMUA VUMBI CAF, SIMBA MMH

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AMPA TANO SIMBU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAAJABU YA DP WORLD SIKU 730 BANDARINI DAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‘MISS WORLD’ KUIPAISHA TANZANIA DUNIANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?