• ePaper
Monday, April 20, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MWIGULU AKOMAA NA WAKANDARASI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 20, 2026
in Habari, Kitaifa
0
MWIGULU AKOMAA NA WAKANDARASI
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na SELINA MATHEW, DODOMA

WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, ameweka jiwe la msingi mradi wa maji wenye thamani ya sh. bilioni 17.5 na kuagiza wakandarasi wanaotekeleza miradi ya maendeleo, wahakikishe wanawalipa wafanyakazi wao stahiki zote bila kuchelewa.

Mradi huo wa maji wa miji 28, unatekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na India.

Akizungumza jijini Dodoma, Dk. Mwigulu alisema serikali haitavumilia vitendo vya wakandarasi kupokea fedha za miradi na kushindwa kulipa wafanyakazi.

Alisema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kufanya hivyo.

“Kazi yangu kubwa kwa wakandarasi ni kuhakikisha kwamba, mnapopokea fedha za mradi, mnawalipa wote wanaofanya kazi.

“Haiwezekani serikali imelipa fedha zote halafu wale waliotekeleza mradi wanabaki wanahangaika kudai haki zao,”alisema.

Alisema serikali itaanza kuwachukulia hatua za kisheria wakandarasi watakaobainika kufanya udanganyifu huo, ikiwa ni pamoja na kuwaorodhesha katika orodha ya watu wasiostahili kupewa kazi za serikalini.

“Tutakapokuta mkandarasi amelipwa fedha zote za mradi, lakini hajawalipa wafanyakazi wake, hilo tutalichukulia kama utapeli.

“Watu wa aina hiyo, hawataruhusiwa kufanya kazi tena ndani ya nchi yetu,” alisema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimpongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa jitihada zake za kuhakikisha upatikanaji majisafi na salama unaimarika nchini.

Alisema maji ni huduma muhimu isiyoepukika kwa maisha ya kila siku.

“Rais amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha miradi ya maji inatekelezwa.

“Ukweli ni kwamba, maji hayana mbadala, hayana ibada, kila mtu anahitaji maji bila kujali eneo au aina ya chakula,” alisema.

Aliipongeza Wizara ya Maji na wataalamu wake kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo, akisema ufuatiliaji wa karibu umeondoa kasoro zilizokuwa zikijitokeza awali, ikiwemo miradi hewa na visima visivyofanya kazi.

Alibainisha kuwa, serikali itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana na wananchi wanapata huduma stahiki.

Alisema kukamilika kwa mradi huo ni hatua muhimu katika kutatua changamoto ya upatikanaji maji katika eneo husika, akisisitiza kuwa, tatizo hilo linaelekea kumalizika kabisa.

“Ninaamini kabisa tatizo la maji linakwenda kumalizika kwa kiwango kikubwa kutokana na jitihada hizi zinazoendelea,” alisema.

Katika hatua nyingine, Dk. Mwigulu alisema ataendelea kuwashughulikia watumishi na viongozi wanaofuja fedha za umma hadi wajute, akisisitiza hakuna atakayevumiliwa katika suala hilo.

Alisema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Msanga, Chamwino.

“Nitashughulika na wanaofuja fedha mpaka watajuta kuzaliwa. Mnaosema hii ni nguvu ya soda, mtajuta,”alisisitiza.

Dk. Mwigulu alieleza kuwa, serikali imetoa fedha nyingi za maendeleo ambazo hazijawahi kutolewa kwa kiwango hicho tangu uhuru wa nchi, hivyo ni wajibu wa viongozi na watendaji kuhakikisha zinasimamiwa ipasavyo na kuwanufaisha wananchi.

Waziri Mkuu alisema haiwezekani fedha zinapelekwa katika miradi ya maendeleo hadi ngazi ya wilaya na vijiji, baadhi ya watendaji wanakosa uadilifu na kuanza kuzitumia vibaya.

Alisisitiza kuwa, hatasita kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kufanya ubadhirifu, akisema tayari amekuwa akifuatilia utekelezaji wa maagizo ya serikali katika maeneo mbalimbali nchini.

Waziri Mkuu alisema dhamira ya Rais ni kuona Watanzania wanapata tabasamu kupitia huduma bora za kijamii, hivyo jukumu lake kikatiba ni kusimamia shughuli za serikali na kuhakikisha maagizo ya Rais yanatekelezwa kikamilifu.

Kuhusu migogoro ya ardhi, Waziri Mkuu alisema sehemu kubwa ya malalamiko aliyoyapokea yanatoka kwa wananchi na  kuwataka maofisa ardhi kuwajibika ipasavyo na kushughulikia kero hizo kwa haraka.

Pia, aliwataka Watanzania kuendelea kulinda amani na umoja wa nchi, akisema kuna baadhi ya watu wasioitakia mema Tanzania wanaotamani kuona wananchi wakigawanyika wanufaike na rasilimali za taifa.

Aliahidi serikali itaendelea kusimamia kwa karibu matumizi ya rasilimali za nchi na kuhakikisha zinawanufaisha wananchi, huku akionya hakuna msamaha kwa atakayebainika kuhujumu jitihada hizo.

JUMAA AWESO

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, alisema wananchi wanapaswa kumshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuwekeza fedha nyingi katika miradi ya maji.

Alisisitiza kuwa, sekta hiyo ni muhimu kwa maisha ya kila siku, kwani maji hayana mbadala wala hayana ubaguzi wa matumizi.

Waziri huyo, alisema mradi huo wa zaidi ya sh. bilioni 17.2 ni ushahidi wa dhamira ya serikali ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ya maji, tofauti na ilivyokuwa awali, baadhi ya maeneo yalikuwa yakikabiliwa na uhaba wa huduma hiyo.

Aweso alimpongeza Waziri Mkuu kwa usimamizi wake wa karibu wa miradi ya maendeleo, akibainisha kuwa, hatua hiyo imeongeza uwajibikaji na kuondoa miradi hewa.

“Kwa muda mfupi tangu aaminiwe, Waziri Mkuu amekuwa mstari wa mbele kufuatilia utekelezaji wa miradi na kuhakikisha fedha za umma zinaleta matokeo halisi,” alisema.

Alisema kwa ujio wake mradi huo, umeleta matumaini makubwa kwa wananchi wa Chamwino na maeneo jirani.

MHANDISI CHARLES MAFIE

Awali, akiwasilisha taarifa ya mradi, Mkurugenzi wa Usambazaji Maji wa wizara hiyo, Mhandisi Charles Mafie, alisema mradi huo utaongeza upatikanaji maji kutoka lita milioni 4.2 hadi lita milioni 7.7 kwa siku, umefika asilimia 70 na ukikamilika Agosti, utanufaisha wananchi 60,000 wa Kata za Chamwino, Buigiri, Msanga na Mtumba.

“Kupitia mradi huu, hali ya upatikanaji wa maji utaongezeka kutoka asilimia 91 hadi 100, sababu tutakuwa na ziada ya lita milioni 2.7,” alisema.

WANANCHI WANENA

Mkazi wa Chamwino, Jemima John, alisema mradi huo, utakuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi, kwa muda mrefu, wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji majisafi na salama, hali iliyowalazimu kutembea umbali mrefu kuyatafuta.

Alieleza kuwa, kukamilika kwa mradi huo kutarahisisha maisha yao ya kila siku na kuwaondolea adha waliyoizoea kwa miaka mingi.

Naye, Mariam Nyembela, alisema upatikanaji wa maji ya uhakika utasaidia kuboresha afya za wananchi pamoja na kupunguza muda unaotumika kutafuta maji, hasa kwa wanawake na watoto.

Alifafanua kuwa, mradi huo utaleta maendeleo kwa jamii kwani wananchi wataweza kujikita zaidi katika shughuli za uzalishaji, badala ya kupoteza muda mwingi kusaka maji.

Kwa upande wake, Julias Magana, alisema mradi huo, utachochea maendeleo ya kiuchumi katika eneo hilo kwa kuwa, maji ni hitaji muhimu katika shughuli za kijamii na kiuchumi.

Alisema kuwa, kuondoka kwa changamoto ya maji kutawawezesha wananchi kufanya shughuli zao kwa ufanisi zaidi na kuinua kipato chao.

Previous Post

AJIRA 45,000 ZANUKIA

Next Post

WANASIASA WATAJA FAIDA ZA MUUNGANO

Next Post
WANASIASA WATAJA FAIDA ZA MUUNGANO

WANASIASA WATAJA FAIDA ZA MUUNGANO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA, DK. NCHIMBI WAIMWAGIA SIFA STARS

RAIS DK. SAMIA, DK. NCHIMBI WAIMWAGIA SIFA STARS

4 months ago
BALOZI NCHIMBI AMSIFU DK. SAMIA KUIMARISHA UHUSIANO

BALOZI NCHIMBI AMSIFU DK. SAMIA KUIMARISHA UHUSIANO

8 months ago

Popular News

  • SIMBA KASI ILE ILE

    SIMBA KASI ILE ILE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DAKTARI ATAJA DALILI ZA SHINIKIZO LA DAMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WANASIASA WATAJA FAIDA ZA MUUNGANO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU AKOMAA NA WAKANDARASI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • AJIRA 45,000 ZANUKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?