• ePaper
Tuesday, April 21, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RAIS DK. SAMIA ABADILI MATUMIZI YA FEDHA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 21, 2026
in Habari, Kitaifa
0
RAIS DK. SAMIA ABADILI MATUMIZI YA FEDHA
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI MAALUMU

WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ameelekeza fedha zilizokuwa zimepangwa kugharamia maadhimisho ya Sherehe za Muungano mwaka huu, zitumike kukarabati miundombinu ya barabara zilizoharibiwa na mvua inayoendelea kunyesha nchini.

Alisema hayo jijini Dodoma, ofisini kwake Mlimwa, alipouarifu umma kuhusu maadhimisho ya Miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakavyofanyika.

“Maadhimisho ya sherehe za miaka 62 ya Muungano, yatafanyika katika ngazi ya mikoa yote nchini, ambapo viongozi wakuu wa Kitaifa, watafanya shughuli za kutembelea, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi ya maendeleo,” alisema.

Aidha, Dk. Mwigulu alisema imeelekezwa kuwa, wakuu wa mikoa watembelee, waweke mawe ya msingi na kuzindua miradi ya maendeleo pamoja kushiriki shughuli za usafi wa mazingira, kupanda miti na kufanya mashindano ya michezo mbalimbali.

“Ninamshukuru Rais Samia kwa kuelekeza fedha ambazo zingetumika kwa kufanya maadhimisho haya kwa gwaride na michezo ya halaiki, zitumike katika shughuli nyingine za maendeleo, ukiwemo ukarabati wa miundombinu ya barabara zilizoharibiwa na mvua inayoendelea kunyesha nchini,” alisema.

Pia, Waziri Mkuu aliagiza majengo yote ya serikali kunakshiwa kwa rangi za Bendera ya Taifa kuanzia jana hadi Aprili 26, mwaka huu, siku ya kilele. 

“Majengo yote ya Serikali Tanzania Bara, yapambwe kwa vitambaa vya rangi ya Bendera ya Taifa, picha za waasisi wa Muungano na picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema.

Aliongeza kuwa, upande wa Zanzibar, majengo yapambwe kwa vitambaa vya rangi sahihi za Bendera ya Taifa, picha za waasisi wa Muungano na picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na picha ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

“Nitumie fursa hii kuwahamasisha wananchi wote kushiriki ipasavyo katika shughuli za kijamii, midahalo na makongamano katika kila mkoa, kujadili maendeleo endelevu yaliyofikiwa na nchi yetu kipindi cha miaka 62 ya muungano.

Aidha, ni muhimu Wananchi wote waendelee kuulinda uungano wetu kudumisha umoja, amani na mshikamano wetu,” alihimiza.

Shughuli nyingine zitakazoambatana na maadhimisho hayo ni pamoja na mashindano ya michezo na sanaa mbalimbali, mashindano ya uandishi wa insha kwa shule za msingi na sekondari; mahojiano maalumu na wazee maarufu, midahalo na makongamano kuhusu Muungano na hatua ya maendeleo iliyofikiwa hadi hivi sasa.

Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni Miaka 62 ya muungano: amani, umoja na mshikamano ni msingi wa maendeleo endelevu.

WADAU WANENA

Wadau wa maendeleo na wanasiasa, waliipongeza serikali kwa uamuzi wake wa kuzielekeza fedha za maadhimisho hayo zitumike kutekeleza miradi ya maendeleo nchini.

ABDUL KAMBAYA

Mdau wa maendeleo nchini, Abdul Kambaya, alisema huo ni uamuzi mzuri ulifanywa na serikali wa kwenda kujenga barabara nchini.

Alisema inatambulika hivi sasa serikali ipo katika utekelezaji wa barabara nyingi nchini, fedha hizo zitakwenda kujenga miundombinu hiyo.

“Naipongeza serikali kwa hatua hiyo ya kuchukua fedha za sherehe za Muungano na kwenda kutekeleza miradi ya kimaendeleo kama ujenzi wa barabara nchini,”alisema.

Alisema ni wazi inaonekana kuwa, Rais Dk. Samia ni kiongozi anayeendeleza yale yalioachwa na Hayati Rais Dk. John Magufuli na kuanzisha mengine ambayo yana manufaa kwa taifa.

“Tunaona wazi Rais Dk. Samia anavyofanya kazi zake katika uongozi wenye maono kwa sababu, ameendeleza miradi mingi ambayo ina manufaa kwa taifa letu ikiwemo Bwawa la Mwalimu Nyerere na ujenzi wa madarasa kwa shule za msingi na sekondari,”alisema.

HASSAN DOYO

Aliyekuwa mgombea Urais wa Chama cha NLD, Hassan Doyo, alisema serikali inatekeleza yale mambo yenye manufaa kwa taifa.

“Nakumbuka Hayati Rais Dk. John Magufuli, alishawahi kuelekeza fedha za sikukuu ya Muungano zijenge kipande cha barabara ya Bagamoyo kutoka Morocco hadi Mwenge na ilifanyika hivyo na Watanzania tunapenda maendeleo kama hayo,”alisema.

Previous Post

SIMBA KASI ILE ILE

Next Post

NEEMA YAJA, MIKAKATI HADHARANI KUINUA VIJANA

Next Post
NEEMA YAJA, MIKAKATI HADHARANI KUINUA VIJANA

NEEMA YAJA, MIKAKATI HADHARANI KUINUA VIJANA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TRA YANG’ARA ROBO YA TATU:MAKUSANYO YAVUKA MALENGO KWA KASI YA AJABU

TRA YANG’ARA ROBO YA TATU:MAKUSANYO YAVUKA MALENGO KWA KASI YA AJABU

3 weeks ago
VIJUE VIGOGO SABA VITAKAVYOTIKISA AFCON NA KOMBE LA DUNIA

VIJUE VIGOGO SABA VITAKAVYOTIKISA AFCON NA KOMBE LA DUNIA

4 months ago

Popular News

  • MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

    MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‘MISS WORLD’ KUIPAISHA TANZANIA DUNIANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BIL. 195.66/- KUJENGA BONDE MTO MSIMBAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ULEGA AJIBU MAPIGO KUHUSU MTANDAO WA BARABARA NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NEEMA YAJA, MIKAKATI HADHARANI KUINUA VIJANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?