• ePaper
Saturday, October 24, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WAZIRI MKUU ATETA NA MAKAMU WA RAIS WA IFAD

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 21, 2026
in Habari, Kitaifa
0
WAZIRI MKUU ATETA NA MAKAMU WA RAIS WA IFAD
0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI MKUU Dk. Mwigulu Nchemba, amekutana na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Dk. Geraldine Mukeshimana na kujadiliana naye masuala ya kilimo, uvuvi na uchumi wa bluu.

Mazungumzo hayo yalifanyika kando ya Mkutano wa Kimataifa wa Norman E. Borlaug (Borlaug Dialogue) ulioanza Oktoba 20, 2026 katika Kituo cha Mikutano cha Iowa, jijini Des Moines, Marekani.

Katika majadiliano yao, Waziri Mkuu alimshukuru Dk. Mukeshimana kwa ufadhili unaotolewa na IFAD kwenye uvuvi wa bahari kuu chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na uendelezaji wa uchumi wa bluu kupitia Wizara ya Uchumi wa Bluu na Uvuvi ya Zanzibar.

“Hii miradi ni ya muhimu na inapewa kipaumbele zaidi kwani inasaidia kuzalisha ajira kwa wanawake na vijana,” amesema.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa IFAD, Dk. Mukeshimana aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuwa kitovu cha upatikanaji wa chakula kwa maeneo yanayoizunguka.

“Binafsi ninawapongeza kwa sababu mmeendelea kuwa kitovu cha uzalishaji wa chakula cha uhakika barani Afrika. Mnafanya kazi kubwa na nzuri mno ya kulisha chakula kwenye maeneo ya jirani,” amesema.

Kipekee, Dk. Mukeshimana amemsifu Dk. Mwigulu akisema: “Tanzania imebahatika sana kupata Waziri Mkuu ambaye zamani alishawahi kuwa Waziri wa Kilimo na baadaye akawa Waziri wa Fedha. Siyo kila nchi imepata bahati kama hiyo, Tanzania mmebarikiwa sana.”

Amesema taasisi hiyo itaendelea kufadhili miradi inayolenga kuondoa njaa na umaskini kwa kuwekeza kwa watu wa vijijini, kuwezesha ushiriki wao katika masoko na kuimarisha ustahimilivu wa hali ya hewa wa maisha yao.

Waziri Mkuu ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Ngwaru Maghembe, Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde, Balozi wa Tanzania Washington, Elsie Kanza na watendaji wengine wa Serikali.

Previous Post

YANGA, SIMBA UBABE UBABE CAFCL

Next Post

DOUMBIA AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO

Next Post
DOUMBIA AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO

DOUMBIA AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. NCHIMBI : WANANCHI MIKOA 11 KUMPA RAHA DK. SAMIA

DK. NCHIMBI : WANANCHI MIKOA 11 KUMPA RAHA DK. SAMIA

1 year ago
SIMAMIENI HAKI

SIMAMIENI HAKI

9 months ago

Popular News

  • TANZANIA YALENGA KUWA MZALISHAJI  BORA WA CHAKULA DUNIANI

    TANZANIA YALENGA KUWA MZALISHAJI  BORA WA CHAKULA DUNIANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TAASISI 2,682 ZAANZA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA, SERIKALI YALENGA TAASISI 30,000

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA KUWA KITOVU SOKO LA KABONI AFRIKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA URATIBU WA MAFUNZO TARAJALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UKURASA MPYA BIMA YA AFYA KWA WOTE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?