• ePaper
Saturday, June 13, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

SERIKALI YAOMBA KUENDELEZA USHIRIKIANO NA IRELAND KUPITIA AWAMU YA PILI YA MRADI WA MAZIWA FAIDA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
June 12, 2026
in Habari, Kitaifa
0
SERIKALI YAOMBA KUENDELEZA USHIRIKIANO NA IRELAND KUPITIA AWAMU YA PILI YA MRADI WA MAZIWA FAIDA
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeomba kuendelezwa kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Ireland kupitia utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mradi wa Maziwa Faida kuanzia mwaka 2027 hadi 2032, ili kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika kuongeza uzalishaji wa maziwa, kuboresha tija na kuinua maisha ya wafugaji nchini.

Ombi hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Fabian Madele, wakati akifungua rasmi Maonesho ya Ubunifu na Teknolojia katika Sekta ya Maziwa (TALIRI Open Day 2026) yaliyofanyika katika Kituo cha Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Kanda ya Mashariki, jijini Tanga.

Dkt. Madele alisema Mradi wa Maziwa Faida unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania kupitia TALIRI na Taasisi ya Maendeleo ya Kilimo na Chakula ya Ireland (TEAGASC), kwa ufadhili wa Serikali ya Ireland kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania, umeleta mabadiliko makubwa katika sekta ya maziwa, hasa Mkoa wa Tanga.

Alieleza kuwa kabla ya kuanza kwa mradi huo, wafugaji wengi walikuwa wakizalisha wastani wa lita tatu hadi tano za maziwa kwa ng’ombe mmoja kwa siku. Hata hivyo, kupitia matumizi ya teknolojia bora za ufugaji, malisho ya kisasa, huduma za ugani zilizoimarishwa pamoja na mafunzo kwa wafugaji, uzalishaji umeongezeka hadi wastani wa lita 15 kwa ng’ombe mmoja kwa siku katika maeneo mengi yaliyofikiwa na mradi.

“Matokeo haya yanaonesha wazi mchango mkubwa wa utafiti, ubunifu na ushirikiano wa kimataifa katika kuongeza tija, kuboresha kipato cha wafugaji na kuimarisha usalama wa chakula na lishe nchini,” alisema Dkt. Madele.

Aidha, alisema Tanzania kwa sasa inazalisha takribani lita bilioni 4.1 za maziwa kwa mwaka huku mahitaji ya taifa yakikadiriwa kufikia lita bilioni 13 kwa mwaka, hali inayoashiria uwepo wa fursa kubwa ya kuwekeza zaidi katika sekta ya maziwa ili kupunguza pengo la uzalishaji na kuongeza mchango wa sekta hiyo katika uchumi wa taifa.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Bi. Suzanne Keatinge, aliipongeza TALIRI kwa utekelezaji mzuri wa mradi huo na kuwatambua watafiti, maafisa ugani pamoja na wadau mbalimbali waliochangia mafanikio yake.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TALIRI, Prof. Erick Komba, aliishukuru Serikali ya Ireland kwa ufadhili wake na kueleza kuwa mafanikio yaliyopatikana katika Awamu ya Kwanza ya Mradi wa Maziwa Faida (2021/2022–2025/2026) yameweka msingi imara wa kuendelea kuleta mageuzi chanya katika sekta ya maziwa nchini.

Prof. Komba alisema TALIRI itaendelea kuhakikisha kuwa matokeo ya tafiti, ubunifu na teknolojia zilizozalishwa kupitia mradi huo zinawafikia wafugaji wengi zaidi ili kuongeza uzalishaji, tija na ushindani wa sekta ya maziwa.

Aliongeza kuwa mradi huo uliogharimu zaidi ya Euro milioni 3, sawa na zaidi ya Shilingi bilioni 7 za Kitanzania, umenufaisha zaidi ya wanawake na vijana 3,000 katika ukanda wa pwani ya mashariki, hususan Wilaya ya Muheza mkoani Tanga.

Kwa mujibu wa Prof. Komba, mafanikio mengine ya mradi huo ni pamoja na kufanya tafiti za malisho bora yanayostahimili mazingira ya ukanda wa pwani, kubaini aina bora za ng’ombe wa maziwa, kuwajengea uwezo maafisa ugani, kutoa mafunzo kwa wafugaji, kuimarisha vyama vya ushirika vya wafugaji, kuboresha miundombinu ya utafiti na kuanzisha mashamba darasa yanayotumika kusambaza teknolojia za kisasa za ufugaji.

Mradi wa Maziwa Faida umetajwa kuwa mfano wa mafanikio wa ushirikiano wa maendeleo unaochochea matumizi ya utafiti, ubunifu na teknolojia katika kutatua changamoto za uzalishaji wa maziwa na kuchangia ukuaji endelevu wa sekta ya mifugo nchini Tanzania.

Previous Post

BAJETI YA KUJITEGEMEA

Next Post

NI MWENDO WA KIDIGITALI, SUKARI SASA KUCHANGIA BIMA YA AFYA

Next Post
NI MWENDO WA KIDIGITALI, SUKARI SASA KUCHANGIA BIMA YA AFYA

NI MWENDO WA KIDIGITALI, SUKARI SASA KUCHANGIA BIMA YA AFYA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WATAALAMU WATAJA MAMBO 8 KUEPUKA UHABA WA MAJI DAR

WATAALAMU WATAJA MAMBO 8 KUEPUKA UHABA WA MAJI DAR

6 months ago
NEEMA ZAIDI SEKTA KILIMO

NEEMA ZAIDI SEKTA KILIMO

4 months ago

Popular News

  • AFRIKA KUCHOCHEA UTUNZAJI MAZINGIRA KUPITIA NISHATI SAFI

    AFRIKA KUCHOCHEA UTUNZAJI MAZINGIRA KUPITIA NISHATI SAFI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWAKINYO AOMBA RADHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, SIMBA NI KIVINGINE ZAIDI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MEXICO YAANZA KWA KISHINDO WC, KADI ZATEMBEA HATARI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NI MWENDO WA KIDIGITALI, SUKARI SASA KUCHANGIA BIMA YA AFYA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?