• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

UWANJA WA BENJAMIN MKAPA WAFIKIA 90%

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 3, 2025
in Burudani, Michezo
0
UWANJA WA BENJAMIN MKAPA WAFIKIA 90%
0
SHARES
12
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na VICTOR MKUMBO

UKARABATI wa Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam umefikia asilimia 90% kukamilika hivi sasa.

 Kwa mujibu wa Mratibu wa Viwanja nchini, Milinde Mahona ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa, umefikia asilimia 90 kukamilika.

Alisema hivi sasa zimebakia asilimia 10 kuhakikisha uwanja huo unakamilika na ambapo unatarajiwa kutumika katika michuano mbalimbali ikiwemo Kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2027).

“Hivi sasa Uwanja wa Benjamin Mkapa tayari umeshakamilka kwa asilimia 90 na kwamba zimebakia asilimia 10.

“Ukarabati unakwenda vizuri tuna imani utakamilika kwa wakati kwani ni moja ya viwanja vitakavyotumika katika michuano ya AFCON 2027 ambapo Tanzania tutakuwa wenyeji kwa ushirikiano wa nchi za Kenya na Uganda,” alisema Mahona.

Alisema ukarabati wa uwanja huo umefanyika katika maeneo mbalimbali yakiwemo uwanja (pitch), kufunga viti vipya, kufunga taa ndani na nje na sehemu ya kukaa waandishi wa habari.

Alisisitiza kwa upande wa ujenzi wa Uwanja wa kisasa wa mpira wa soka Arusha, hivi sasa unandelea kufanyika kwa kasi ambapo umefikia asilimia 66.

Alisema awali Oktoba, mwaka huu ujenzi wa uwanja huo ulikuwa umefikia asilimia 63.5.

Uwanja huo ambao upo katika eneo la Olomoti, Arusha ukikamilika unatarajiwa kuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 30,000.

“Ujenzi wa Uwanja Arusha unaendelea kwa kasi ambapo hivi sasa umefikia asilimia 66.

Alisema uwanja huo utamilika kwa wakati kuhakikisha unatumika katika fainali za michuano AFCON 2027 na mashindano mbalimbali.

“Mafundi wanaendelea kufanya kazi kwa kasi na hivi sasa ujenzi wa uwanja wa Arusha umeshafikia asilimia 66.

“Hivi sasa mafundi wameshaanza kuchimba eneo la kuchezea mpira ‘pich’ huku maeneo mengine yakiwa tayari yamekamilika yakiwemo majukwaa ya watazamaji.

“Mbali ya kuanza kuchimba eneo la kuchezea, maeneo mengine ambayo yanafanyiwa kazi kwa ubunifu ni paa la uwanjani, ufungaji wa miundombinu ya umeme, zimamoto, TEHAMA na kuweka mabomba,” alisema.

Mratibu Mahona, alisema kukamilika kwa uwanja huo utalenga kuongeza miundombinu ya michezo nchini na kupanda kwa hadhi kutokana na ubora wake.

“Pia mafundi wanaendelea kufanya kazi kwa bidii huku nje ya uwanja ujenzi ukiendelea ikiwemo maeneo ya kuegeshea magari,” alisema.

Aliongeza kwa upande wa Uwanja wa soka wa Dodoma, hivi sasa wameshaanza kusafisha eneo na baadaye ujenzi utaanza mara moja.

Ujenzi wa Uwanja wa Arusha, Dodoma na ukarabati wa Benjamin Mkapa na Uhuru ni juhudi za Serikali chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha michezo inafanyika katika miundombinu bora zaidi.

Previous Post

MAGOLI AFUNGUKA SIMBASC

Next Post

SIMBASC NJIA HII HAPA MAKUNDI KIMATAIFA

Next Post
SIMBASC NJIA HII HAPA MAKUNDI KIMATAIFA

SIMBASC NJIA HII HAPA MAKUNDI KIMATAIFA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

NDEJEMBI ATAJA VIPAUMBELE 10 SEKTA YA NISHATI

NDEJEMBI ATAJA VIPAUMBELE 10 SEKTA YA NISHATI

3 months ago
TAIFA STARS KUKIPIGA FIFA SERIES 2026

TAIFA STARS KUKIPIGA FIFA SERIES 2026

5 months ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?