• ePaper
Monday, May 25, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

VIJANA LINDENI AMANI YA NCHI – DK. MIGIRO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 5, 2025
in Habari, Kitaifa
0
VIJANA LINDENI AMANI YA NCHI – DK. MIGIRO

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Asha-Rose Migiro

0
SHARES
14
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Dodoma
NA SELINA MATHEW

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Asha-Rose Migiro, ametoa wito kwa vijana kuilinda nchi yao kwa kuhakikisha matukio yaliyojitokeza Oktoba 29 mwaka huu wakati wa uchaguzi mkuu, hayajirudii.

Amesema matukio hayo yaliyochafua taswira ya Tanzania siyo utamaduni wa Taifa na  hayaakisi maisha ya wananchi.

Balozi Dk. Migiro aliyasema hayo jijini hapa, alipofungua kongamano la Jukwaa la Wanawake 2025 lililoambatana na kauli mbiu isemayo “Mama ni Amani.”

Katika kongamano hilo lililowakutanisha washiriki zaidi ya 2000 kutoka maeneo mbalimbali nchini, Dk. Migiro alisema wanawake wana mchango wa kipekee kuhakikisha nchi hairudi katika changamoto zilizojitokeza Oktoba 29 mwaka huu.

“Sisi wanawake tuna mchango wa pekee na ili kuhakikisha kwamba haturudi tena katika changamoto ile, tutoe mawazo chanya ambayo yatatutoa hapa tulipo kuendelea mbele kuwezesha Taifa kuendelea kuwa salama.

Alisisitiza: “Siyo utamaduni wetu, siyo hulka wala maisha ambayo sisi Tanzania tumekuwa tukiishi yaliyotupatia sifa kubwa duniani kuwa nchi ya kisiwa cha amani na utulivu, tufanye kila tuwezalo kurejea tena katika nafasi yetu ambayo itaifanya nchi iendelee kuwa kiongozi katika amani, utulivu na maendeleo.”

“Tumeona changamoto zilizotokea, namna ambavyo serikali imesimama imara kuhakikisha kwamba utulivu unarejea katika nchi yetu, shughuli za usalishaji ambazo ziliathiriwa na changamoto hiyo zimeaanza tena,” alibainisha.

Alisema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji falsafa ya 4R ambayo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amekuwa akiisisitiza kwa kubeba mambo manne likiwemo suala la ustahimilivu.

Alibainisha kuwa kupitia falsafa hiyo,  Rais Dk. Samia alieleza nchi ipo tayari kujijenga upya, kuimarisha mazuri yaliyopo na ndiyo sababu jukwaa hilo limewaleta wanawake na vijana wenye mirengo mbalimbali.

“Kwa sababu inapokuja katika Tanzania ni yetu wote, sisi wote hatuna sehemu nyingine pa kwenda ila hapa. Kwa mantiki hiyo ujumuishi huu unadhihirisha umuhimu kwamba tufanye kila tuwezalo kuhakikisha kwamba haturudi nyuma, haturudi katika changamoto zile,” alisisitiza.

Kuhusu tume iliyoundwa na Rais Dk. Samia kuchunguza kiini cha vurugu zilizojitokeza siku ya Uchaguzi Mkuu, Dk. Migiro alisema ni mwanzo mzuri kuelekea mchakato wa kuimarisha maridhiano.

KATE KAMBA

Kwa upande wake, mwanasiasa mashuhuri nchini, Kate Kamba aliwasilisha mada kuhusu nafasi ya mwanamke katika kulinda amani.

Mwanasiasa huyo ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, alisema uwekezaji kwa wanawake ni muhimu katika mustakabali wa taifa kwani ni wajenzi wa maadili na amani kuanzia ngazi ya familia.

“Watoto wafundishwe mila, desturi, utambulisho wa jamii ili kuzuia mmomonyoko wa maadili, tusiwaache wafanye vile jamii haitaki,”alisema Kate ambaye ndiye mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo miaka ya 1980.

SIFA SWAI

Akizungumzia athari za kukosekana amani kwa wanawake na jamii, Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Mkoa wa Kilimanjaro, Sifa Swai, alisema kukosekana amani kunaathiri vipato, biashara na maendeleo ya kada mbalimbali.

“Tuhakikishe tunalinda amani kwa nguvu zote, lugha za chuki, matusi vinaweza kuwa chanzo cha mfarakano baina ya watu ndani ya jamii. Vijana wanatumia vibaya mitandao ya kijamii kwa kusambaza jumbe mbaya ambazo zinasambaa haraka, waache, tutunze amani yetu,” alisema Swai ambaye aliwahi kuwa mweka hazina wa kwanza mwanamke ndani ya CCM.

Previous Post

JUKWAA LA WANAWAKE LAIBUKA  NA MAAZIMIO 10 KUHUSU AMANI

Next Post

RAIS DK. SAMIA MGENI RASMI MKUTANO IPU

Next Post
RAIS DK. SAMIA MGENI RASMI MKUTANO IPU

RAIS DK. SAMIA MGENI RASMI MKUTANO IPU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

POINTI UBINGWA YANGA SC KUSAKWA LEO

POINTI UBINGWA YANGA SC KUSAKWA LEO

2 weeks ago
RAIS DK. SAMIA AWAKOSHA VIONGOZI WA DINI NCHINI

RAIS DK. SAMIA AWAKOSHA VIONGOZI WA DINI NCHINI

6 months ago

Popular News

  • WAZIRI MKUU AHIMIZA MALEZI YA KIMAADILI NA USHIRIKIANO WA KIJAMII

    WAZIRI MKUU AHIMIZA MALEZI YA KIMAADILI NA USHIRIKIANO WA KIJAMII

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI MKUU AVITAKA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KUWA MACHO DHIDI YA WAVUNJA AMANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KILIO CHA BANDO CHATUA BUNGENI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ZIARA YA KIHONGOSI YAACHA NEEMA KWA WANAWAKE MARA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA YAJIPANGA KUDHIBITI MIJI HOLELA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?